22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii ya kifugaji yatakiwa kutunza misitu


Na Mwandishi Wetu, Babati 
 
JAMII za wafugaji zimetakiwa kuwekeza katika mazingira kwa kupanda miti kwa ustawi wa viumbe hai ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uhakika wa chakula na nyanda za malisho.
 
Juzi vijiji 13 walikiongozwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani na wenyeviti wa vijiji kutoka wilaya ya Ngorongoro na Babati Vijijini,walikutana wilayani Babati na kupewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa misitu jamii.
  
Akizungumza na wananchi hao kutoka wilaya hizo, Meneja wa Mradi wa uhifadhi na uendelezaji wa ikolojia ya Serengeti kutoka Shirika la Kimataifa la Uhifadhu la  Frankfurt Zoological Society(FZS), Masegeri Tumbuya amesema ipo haja kwa wananchi kutunza mazingira ya misitu kwa maslahi ya sasa na vizazi vijavyo.
 
Amesema kuwa ipo haja kwa jamii kupunguza shughuli za kibinadamu katika maendeo ya misitu na vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa ustawi wa viumbe hai.
 
“Katika hali ya kawaida tumekuwa na changamoto mbalimbali binadamu shughuli za kawaida zinaathiri mazingira tukaona ni vizuri wakati tunajiendeleza kimaisha tutoe elimu ya utunzaji mazingira,”amesema
 
“Ukienda Loliondo mji unakua kwa kasi kubwa,na kwa sababu ya kukua kwa miji yetu inapelekea matumizi ya rasilimali za misitu yanaongezeka yakiongezeka bila mpangilio na kusimamiwa vizuri madhara yakakuwa makubwa,” amesema.
 

Kwa upande wake Mhifadhi misitu kutoka wakala wa misitu Tanzania(TFS),wilaya ya Babati, Paulina Hussein, anasema misitu ya jamii inatoa fursa nyingi ikiwemo za kiafya na uchumi.
 
“Misitu ikisimamiwa vizuri hatutapata madhara kwa sababu jamii imeshatambua umuhimu wa misitu na sisi tutaendelea kutoa elimu kwa jamii kwani wananchi wakishatambua na kuelewa umuhimu wa misitu watatunza na kuhifadhi misitu ikiwemo kupanda miti,”
 
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Ayasanda, Ally Shabani, anaitaka jamii kuhakikisha kila mmoja anakuwa balozi wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya manufaa yao wenyewe ikiwemo upatikanaji wa maji.
 
“Kila mwananchi ni balozi wa kulinda au kuhifadhi mazingira na lazima tuwe waadilifu na niwaombe tukiondoka tukafundishe na wenzetu ili tuweze kushirikiana kuhifadhi mazingira,”ameongeza.

Mmoja wa wananchi hao kutoka Tarafa ya Loliondo,Laloposi Meishook,amesema elimu hiyo itawasaidia sana kwani awali hawakuwa watutunza mazingira ikiwemo misitu hivyo watakuwa mabalozi wa utunzaji wa mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles