29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Niyonzima apigwa ‘stop’ Rwanda

KIGALI, Rwanda

SHIRIKISHO la Soka la Rwanda (FERWAFA) limemsimamisha kuitumikia timu ya taifa kiungo wake, Olivier ‘Sefu’ Niyonzima, kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Hivi karibuni, Niyonzima alicheza na kufunga bao pekee la Rwanda katika kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kenya, mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani huko Qatar.

Licha ya FERWAFA kutoweka wazi sababu ya kumsimamisha, zipo taarifa zinazodai mchezaji huyo hakulala kwenye hoteli waliyofikia Amavubi mjini Nairobi.

“FERWAFA inawataarifu Warwanda wote kwamba Olivier Niyonzima amesimamishwa kuichezea timu ya taifa kwa utovu wa nidhamu,” imesomeka taarifa ya Shirikisho hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles