27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

DC Morogoro aishauri Biko kurudisha kwa jamii

Mwandishi Wetu, Morogoro

Mkuu wa wilaya Morogoro, Albert Msando, ameishauri kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Biko, irudishe faida kidogo kwa jamii ili kuhakikisha nchi inasonga mbele kwa kutumia fursa hiyo ya michezo ya kubashiri.

Msando amesema hayo hayo ofisini kwake wakati anazungumza na mshindi wa sh milioni 10, Luka Lutuli alizoshinda kwenye droo kubwa ya Jumapili iliyopita, ambapo makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika katika banki ya NBC, Tawi la Morogoro Mjini.

Mkuu  huyo wa wilaya, alitumia nafasi hiyo kuipongeza Biko kwa kuendesha bahati nasibu ya wazi inayotoa ushindi wa urahisi ukilinganisha na michezo mingine ya kubahatisha.

“Tunajua Biko mnafanya mchezo mzuri unaotoa fedha kwa Watanzania wote, wakiwapo kutoka mkoani kwetu Morogoro na tukiri hatujawahi kusikia mnalalamikiwa kuhusu kutotoa zawadi zenu, ila ni vyema pia mkarudisha faida kwa jamii ili nchi ijivunie zaidi uwapo wenu,” amesema.

Biko ni mchezo wa kubahatisha unaotoa fedha kwa Watanzania, ambapo zawadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo, zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles