27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Irfan: Tasnia ya mitindo Tanzania bado ipo nyuma

NA JEREMIA ERNEST

MBUNIFU  wa mavazi nchini,  Irfan Riziwanali, amesema Tanzania bado ipo nyuma katika tasnia ya mitindo  pamoja na uwezpo wa vipaji vingi.

Irfani ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alisherekea miaka miwili tangu afungue duka la ubunifu wa mavazi Masaki jijini Dar es Salaam, amesema Tanzania ina wabunifu wengi.

Akizungumza na Mtanzania Digital, amesema wabunifu wa Tanzania wanauwezo mkubwa wa kubuni ila bado tasnia haijapata ushirikiano kutoka katika jamii na taasisi mbalimbali.

“Tumejaliwa uwezo wa kufanya ubunifu tofauti na nchi nyingine katika mavazi lakini bado soko  halijachanganya jamii inapenda vitu vya nje zaidi ndiyo sababu sekta yetu inashindwa kukua kama ilivyo kwa wenzetu,” amesema Irfan.

Katika hafla hiyo Irfan, alitoa nafasi kwa wajasiriamali wa ndani kuuza bidhaa zao katika eneo la duka lake pamoja na kujitangaza kwa wageni na wateja walio hudhuria.

Tofauti na wajasiriamali, wabunifu mashuhuri walijitokeza kumpongeza Irfan kwa kazi kubwa aliyofanya katika tasnia miongoni mwao ni Ally Rehmtulla, Martin Kadinda ,Mustapha Hasanali pamoja na Miss Universe Tanzania 2021, Nelly Kamwelu.

Akizungumza kwa niaba ya waalikwa wengine Ally Rehmtulla amesema kwa kipindi  cha miaka miwili biashara imekuwa ngumu, hivyo anampongeza Irfan, kwa kuweza kupambana.

“Ugonjwa wa korona umekuwa changamoto kwetu wabunifu kwa kukosa wateja kulingana na hali halisi ya uchumi nampongeza Irfan kwa jitihada zake kwa sababu alianza kipindi kigumu lakini amefanikiwa kutengeneza wateja wengi na kuongeza wigo katika biashara yake,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles