27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Lampard arudi, ataka kazi

LONDON, England

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard, anaamini amekaa nje ya kazi kwa muda mrefu, hivyo yuko tayari kurudi kabla ya msimu huu kufikia ukomo.

Lampard mwenye umri wa miaka 43, ambaye aliinoa Chelsea kwa miezi 10 kabla ya kufukuzwa, alikuwa akihusishwa na Crystal Palace, Newcastle na Norwich City, kabla ya timu zote hizo kupata makocha.

Kwa mujibu wa taarifa, huenda safari hii akaibukia kwenye benchi la ufundi la Leicester City kwa kuwa mabosi wa mabosi wa timu hiyo wanahisi kocha wao, Brendan Rodgers, ataondoka.

Hofu ya Leicester kumpoteza Rodgers inakuja baada ya Manchester United kutajwa kuitaka huduma ya kocha huyo ili akakalie kiti cha Ole Gunnar Solskjaer anayeonekana kushindwa kuhimili ushindani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles