26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

NHIF kutatua kero za watoa huduma wa afya

Yohana Paul na Sheila  Katikula, Mwanza

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernad Konga amehaidi kuhakikisha mfuko huo unaendelea kutatua changamoto na kero  kwa wateja wake ikiwemo watoa huduma za afya nchini. 

Konga alisema hayo jana wakati wa  kikao cha watoa huduma wa afya wa serikali na binafsi  kilichofanyika jijini Mwanza ambapo alisisitiza lengo la kikao hicho ni kujadili na kusikiliza changamoto mbalimbali  ili NHIF iweze kutoa mrejesho.

Alisema kuna maboresho yaliyofanywa kwenye mwaka wa fedha  ambayo yanaendana na ilani ya chama cha mapinduzi awamu ya tano kulenga kutambua  changamoto kwa  watoa huduma za afya nchini.
Alisema kulikuwa na   malalamiko ya  kucheleweshwa  malipo ya madai lakini hivi Sasa mfuko umefanya marekebisho katika nyanja mbalimbali  na malipo yanafanyika kwa muda mwafaka  ili waendelee kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF.

“Tumesikia na kupokea malalamiko, tumeshachakata na kuona kama madai hayo ni stahiki na baada ya hapo ifikapo januari 30 ndani ya  siku 14  tunauwezo wa  kuwalipa.

“Tumeanza kwenye hospitali 14 za ngazi mbalimbali Kwa awamu ya kwanza ya majaribio  tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na sasa tunaenda kuifanya nchi nzima ambapo tutafidia madai yao kwa wakati ili waweze kuhudumia wanachama wao.

“Kuna madai ambayo tumepokelea yanaviashilia vya wizi kwani tumebaini zile fedha  ambazo mtoa huduma anadai ni tofauti na huduma aliyotoa  japo siyo kwa wote,” alisema Konga.

Konga liongeza kuwa NHIF imeweka mikakati ya muda mrefu na mfupi kuyafikia makundi yote ikiwemo bodaboda, machinga na wakulima kwani asilimia 70 ya watu nchi nzima ni wakulima  na tayari miongozo tuliyotoa wana uwezo  kukata bima ya mwaka mzima na kuwa na uhakika wa matibabu na afya bora.

Kwa upande wake Meneja wa mfuko wa taifa bima ya afya mkoa wa  Mwanza, Jarlath  Mshashu alisema kiu ya watoa huduma ni kuona uongozi wa mfuko unawatembelea ili waweze kusikiliza matatizo na maelekezo yao na kutambua changamoto walizonazo.

Alisema mfuko huo umeendelea kufanya kazi mbalimbali ikiwamo  kusajili wanachama, kusajili vituo vya kutolea huduma, kukusanya michango kuchakata na kulipa madai ya watoa huduma,kutoa elimu kwa wadau wa mfuko pamoja na kutengeneza kadi za wanachama.

Alisema  kuna vituo zaidi ya 590 vilivyo sajiliwa na mfuko vituo 350 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba 2020 wamesajili vituo vipya 12 zaidi ya vituo 100  vya serikali na vya binafsi vimeweza kufanikisha kurudisha mikataba yao.

Naye, Mkurugenzi  Mtendaji  wa hospitali ya Kamanga Dk  Rodrick Kabangila alisema ucheleweshwaji wa madai ni changamoto hata hivyo ameiomba Nhif kuweza kutatua matatizo yanayozikabili taasisi hizo ili kuendelea kuulinda mfuko huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles