28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Watafiti waja na mbinu ya kuepusha migogoro ya wafugaji

Na Ramadhani Hassan, Kongwa

ILI kuondokana na migogoro ya wakulima na wafugaji imeshauriwa  kupanda majani ya  malisho aina ya Cenchrus Ciliaris kwani yana uwezo wa kustahimili ukame na pia hutumika kipindi cha kiangazi ambacho majani huwa ni shida kwa wafugaji.

Hayo yameelezwa na Mtafiti wa Malisho kutoka Taasisi ya Taifa ya Mifugo (Taliri Kongwa), Dk. George Fupi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati ya ziara iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

COSTECH ilifanya  mafunzo pamoja na ziara ya kuwatembelea watafiti na Taasisi za utafiti  kwa waandishi wa habari za Sayansi katika  mikoa ya Dodoma na Singida.

Dk.Fupi amesema mbegu aina ya Cenchrus Ciliaris wameifanyia utafiti na kugundua inastahimili ukame na ni bora kwa wafugaji kwani majani yake ni bora na hivyo kuifanya  mifugo kuendelea kupata virutubisho muhimu husasani wakati wa kiangazi.

Amesema mbegu hiyo kwa ekari moja ina uwezo wa kutoa tani 4 mpaka 9 hivyo amewashauri wakulima na wafugaji kupanda mbegu hiyo.

“Ushauri wangu kwa wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji nawashauri wapande mbegu hii na kwa sasa watu wanazidi kuongezeka hivyo sehemu za kuchunga zinazidi kupungua,”amesema.

Amezitaja mbegu zingine za malisho  zilizofanyiwa utafiti katika kituo hicho  ni Bathriochloa Inschpta, Eragrostis Superba, Paniciam Maximum na Rhodes grass.

Dk. Fupi pia amesema  wafugaji wanapaswa kuendana na wakati kwa kufuga kisasa na kuondokna na ugugaji holela wa kuhama kutoka sehemu moja na kwenda nyingine kwani kunasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira .

Mtaalam huyo wa malisho anaeleza kuwa ili kuondokana na migongano hiyo,wafugaji wanapaswa kuzingatia kupanda  malisho ya mifugo kwa kuzingatia hali ya hewa ya sehemu husika.

“Malisho ni chakula muhimu sana kwa mifugo, kwa kawaida mifugo hupata chakula hasa nyasi katika malisho ya asili, lakini chakula hiki hakitoshelezi mahitaji kwa kuwa  hakina viinilishe vya kutosha kwa afya bora ya mifugo Kwa mfano, kiasi cha protini na madini ni kidogo ukilinganisha na malisho ya kisasa,”alisema Fupi

Dk. Fupi ameongeza kuwa,mambo makuu mawili kwa mfugaji wa kitanzania yanayomkuba ni mabadiliko ya tabia nchi linalotokana na ongezeko kubwa la watu ambalo linazidi kuimega ardhi ya malisho kwa shughuli mbalimbali kama makazi na kilimo.

Kilimo cha malisho kitapunguza kutembeza mifugo umbali mrefu zaidi kwa ajili ya kutafuta malisho jambo ambalo huharibu ubora wa nyama, hudhoofisha mifugo na kuipunguzia uwezo wa kuzaliana (reproductive efficiency),”anasisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles