26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ndusha ndani Simba ikiivaa Mwadui

ndushaNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba leo inajitupa katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, kucheza na Mwadui FC huku kiungo wa kimataifa wa Congo, Mussa Ndusha, akianza kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tayari Simba imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya Ndusha ambaye anatarajiwa kuanza kwenye mechi hiyo ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Tangu kuanza kwa ligi msimu huu, beki huyo ameonekana kushindwa kufanya kazi iliyomleta Simba kutokana na kukosa ITC.

Ndusha alitua Simba na kupewa mkataba wa miaka miwili, alionekana uwanjani na Simba katika mechi mbili za kirafiki za kimataifa wakati waliposhinda mabao 4-0 dhidi ya AFC Leopard na katika sare ya bao 1-1 dhidi ya URA, zote zilichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba wanaongoza ligi hivi sasa kwa pointi 29 ikiwa imecheza mechi 12, itaingia katika mechi hiyo wakitoka kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans.

Mechi nyingine za ligi hiyo zitakazochezwa leo, Mbeya City wataikaribisha Majimaji katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Ndanda watakuwa ugenini kucheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani huku African Lyon ikiwa wenyeji kwa Tanzania Prisons katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles