25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri amrudisha Pluijm Yanga

pluijmNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

BAADA ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Yanga, Hans van de Pluijm, kuandika barua ya kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, hatimaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameamua kumrudisha kocha huyo ili aendelee kukinoa kikosi hicho.

Pluijm aliandika barua kwa uongozi wa Yanga kujiuzulu baada ya kuletwa kwa kocha Mzambia, George Lwandamina, aliyedaiwa kuingia mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho baada ya kumaliza mkataba wake na Zesco.

Kutokana na kujiuzulu kwa Pluijm, Nchemba aliamua kuingilia kati suala hilo na kufanya mazungumzo na kocha huyo takribani siku tatu ambapo sasa amekubali kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Awali, Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, alianza mazungumzo na wachezaji wa timu kisha kuwashauri viongozi kumrudisha Pluijm kabla ya kuchukua jukumu la kuzikutanisha pande mbili yaani Pluijm na Yanga.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwenye vyombo vya habari ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit jana, hawaoni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo baada ya mafanikio waliyopata.

“Toka umejiunga na Yanga Desemba, 2014 umeisaidia Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili,  Kombe la FA, hivyo hatuoni sababu ya kuachana na wewe,” aliandika Baraka kwenye barua hiyo.

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta Pluijm kujua ameipokeaje barua ya Yanga ya kumtaka kurejea kukinoa kikosi hicho, ambapo alisema kuwa amekubaliana na  maombi ya Waziri Nchemba na hivyo hivi sasa anafungua ukurasa mpya katika kazi yake.

“Nilikwenda kuonana na Nchemba na tumezungumza, kila kitu kimekwenda sawa, nitarudi kuifundisha Yanga na ninafungua ukurasa mpya kwa sasa tunaacha yaliyopita,” alisema Pluijm.

Pluijm alisema tayari aliwaaga wachezaji wa Yanga baada ya kuwasilisha baru ya kujiuzulu kwake na kusababisha kukosekana kwenye mechi ya timu hiyo dhidi ya JKT Ruvu iliyosimamiwa na msaidizi wake, Juma Mwambusi, huku wakishinda mabao 4-0.

Uongozi wa Yanga ulitaka kumwondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa, Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa kocha mkuu, akisaidiwa na wazawa, Charles Mkwasa, Manyika Peter, kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles