23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi za Cecafa zajitutumua Afcon

BADI MCHOMOLO, DAR ES SALAAM

BAADHI ya nchi zinazounda Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), zimeonekana kufanya vema hadi kumalizika kwa raundi ya pili ya mechi za kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 ncihini Gabon.

Licha ya kiwango cha Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kuonekana kuimarika katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Nigeria ‘Super Eagle’, bado imekua moja ya timu ambazo hazijafanya vizuri katika ukanda huo.

Stars ilionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wake mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Nigeria (Super Eagle), mchezo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya 0-0.

Tanzania mpaka sasa kama wengine imecheza michezo miwili na imejikusanyia pointi moja, mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kukubali kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Misri kabla ya sare ya juzi ya 0-0 na Nigeria. Ukilinganisha na nchi nyingine Tanzania imeonekana kuwa haijafanya vizuri.

Tanzania ipo kundi G linaloongozwa na wababe Misri ambao wana pointi sita, wakifuatiwa na Nigeria wenye pointi nne na Tanzania ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja, huku Chad ikiwa haina pointi.

Uganda ambao ndio vinara wa soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, wanaongoza Kundi D wakiwa na pointi 6, kundi hilo linaloundwa na nchi za Burkina Faso, Botswana na Comoros.

Rwanda ambao wako kundi H, wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu, huku kundi hilo likiwa linaongozwa na Ghana kwa pointi sita, nafasi ya tatu inashikwa na Mauritius, Msumbiji ikishika nafasi ya mwisho.

Kundi I, Sudan inashika nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu, kundi linaloongozwa na Gabon wenye pointi nne, nafasi ya tatu ikishikwa na Ivory Coast wenye pointi mbili pamoja na Sierra Leone ambao hawana pointi.

Burundi wao wanashika nafasi ya pili katika kundi K, wakiwa na pointi tatu baada ya kushinda mchezo mmoja, kundi hilo likiongozwa na Senegal ambao wana pointi sita baada ya kushinda michezo yote miwili, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Niger ikifuatiwa na Namibia.

Ethiopia yenye pointi nne kwenye Kundi J, inashika nafasi ya pili kundi likiongozwa na Algeria wakiwa na pointi sita, nafasi ya tatu inashikwa na Seychelles ambao wana pointi moja huku nafasi ya mwisho ikishikwa na Lesotho ambao hawana pointi.

Sudan Kusini imeonyesha kutishia katika kundi C baada ya kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu, katika kundi ambalo linaundwa na mataifa makubwa kama vile Mali, Benin na Equatorial Guinea.

Kenya yenyewe kama Taifa Stars, haijafanya vema sana ipo nafasi ya tatu na ina pointi moja katika kundi E linaloongozwa na Kongo sawa na Guinea-Bissau.

Katika kundi A, Djibouti inashika nafasi ya mwisho, Togo wenye pointi sita ndio wanaongoza wakifuatiwa na Tunisia na Liberia.

Kutokana na hali hiyo, Tanzania bado inahitaji kujituma zaidi katika michezo mingine ijayo, ili kuweza kujihakikishia inasonga mbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles