24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kida Kudz adondosha ‘Figure 8’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MSANII wa muziki nchini Nigeria anayeishi Uingereza, Kida Kudz ameachia singo mpya iitwayo ‘Figure 8’ – Umbo Namba 8, maalumu kwa wanawake wote.

Katika kibao hicho ambacho ameshirikiana na msanii kutoka nchini Italia aitwaye Gemitaiz, Kida Kudz anaonyesha namna alivyo mtundu katika kuandika mashairi yenye mvuto.

Akizungumzia kibao hicho, Kida anasema: “Figure 8 ni ile hali ya kuwa na umbo linalofanana na namba nane. Huu ni wimbo kwa ajili ya wanawake, warembo wazuri. Nimeutengeneza nikiwa chumbani kwangu, nikiwa na mwanangu Solomon pembeni yangu.
“Wakati narekodi huu wimbo, ilikuwa ni wakati wa majira ya joto nchini Uingereza. Sikuandika chochote kabla, nilitiririka tu. Huu ni wimbo maalum kwa ajili ya Afrika na dunia nzima kwa jumla.”

Kida mzaliwa wa Ibadan, Nigeria kwa mama mjasiliamali alifanikiwa kushinda mashindano mbalimbali akiwa na miaka 14 kablabya kuhamia jijini London, Uingereza.

Akiwa nchini Uingereza, alianza masomo ya teknolojia ya muziki, ufundi wa sauti (Audio Engineering), Biashara ya Muziki na utayarishaji kwenye vyombo vya habari katika vyuo vya kati na hatimaye Chuo Kikuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles