23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

NACTE yafuta vyuo 26

dk-adolf-rutayuga-nacte_Na PATRICIA KIMELEMETA – DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), limefuta vyuo 26 vilivyokuwa vinatoa masomo ya ufundi, huku vingine 20 vikisimamishiwa programu zisizosajiliwa na baraza hilo.

Pia baraza hilo limesimamisha vyuo viwili baada ya kubainika havijasajiliwa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk. Adolf  Rutayuga, ilisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini makosa  mbalimbali, yakiwamo ya kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa.

Ilisema baraza hilo limekuwa likifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa kwa kipindi kirefu.

“Kama ilivyoelezwa katika sheria za usajili na kanuni za leseni, kutozingatia matakwa yoyoye yaliyowekwa na baraza, ni kosa kisheria. Kanuni zinasema hatua kali zinaweza kuchukuliwa kwa kila kosa. Kulingana na matokeo ya ufuatiliaji uliofanywa na timu maalumu, baraza lina uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya taasisi au vyuo vinavyoshindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa.

“Baada ya kufanya utafiti, tulibaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na baraza katika cheti cha usajili, vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika na vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema baraza hilo limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo vya ufundi 48.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles