BAADA ya Dk Tulia kushinda nafasi ya Naibu Spika, mwigizaji mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael (Lulu) ameandika katika ukurasa wake wa Instagram akimpongeza kutokana na elimu yake ambayo anaamini ndiyo iliyompeleka katika nafasi hiyo ya Unaibu Spika.
“Kusoma kuzuri jamani, wakati wakina nanii wanaendelea kunyooshana Insta, watu na elimu zao wananyoosha kwenye vyenye maana, dada Tulia hapo kanyoosha kwenye Unaibu Spika bila hata ya wigi wala ‘make up’, sema nami siko mbali ipo siku Magogoni kutazaa matunda, haya bisheni na huyo ndiyo Naibu Spika,’’ alimaliza kuandika hivyo.