28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Salabi: Wakenya ‘hawasapoti’ wasanii wao

NA MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI wa muziki wa asili kutoka Kenya, Mandela Salabi, amewataka mashabiki na wadau wa muziki wa Kenya kuwatia moyo wasanii wao wanapotumbuiza katika matamasha ya nchini humo kama wafanyavyo Watanzania kwa wasanii wao.

Salabi amesema mashabiki wa muziki nchini Kenya wengi wao hawatoi hamasa wala hawajali wakifanyacho wasanii wao katika maonyesho yao tofauti na mashabiki wa Tanzania wakati wote huonekana kuvutiwa na kifanywacho na wasanii wao jukwaani.

“Kwetu Kenya tuna tatizo kubwa la mashabiki kutokujali muziki na wasanii wao, lakini kila ninapokuja kutumbuiza Tanzania huwa nafurahi kwa kuwa mashabiki wanakubali ninachofanya jukwaani wananisikiliza, wanacheza pamoja nami na pia wanafuata ninachowataka wafanye, tena kwa furaha tofauti na mashabiki wa Kenya,’’ alieleza Salabi, ambaye pia alitumbuiza katika tamasha la Karibu Festival lililofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles