27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamitindo Emanuel Ek ‘Kingof Arizona’ awatamani Jux, Calisah

Phoenix Marekani

TASNIA ya mitindo imeendelea kukua kwa kasi ulimwenguni kote huku ikitoa fursa kwa vijana mbalimbali kujiajiri kwenye sanaa hiyo.

Miongoni mwa vijana kutoka Afrika Mashariki wanaoishi Marekani na kufanya kazi ya mitindo ni Emanuel Ek, mwanamitindo anayekuja kwa kasi kutoka Phoenix, Arizona.

Emanuel Ek amefanya mahojiano haya na mtanzania.co.tz ili mashabiki wa mitindo katika ukanda huu waweze kumfahamu na kufuatilia kazi zake za mitindo.

SWALI: Emanuel Ek ni nani na uliingia vipi kwenye tasnia ya mitindo?

Emanuel Ek: Mimi ni kijana wa kiafrika ambaye nipo hapa Arizona Marekani  na kwa upande wa fasheni, binafsi nilikuwa napenda tangu nikiwa mdogo na nilipopata nafasi ya kuingia kwenye sanaa nilifurahi maana ilikuwa ni ndoto yangu.

SWALI: Changamoto zipi unapitia kwenye kazi zako za mitindo?

 Emanuel Ek: Changamoto zipo nyingi sababu hii tasnia ni kubwa na kila mwanamitindo anatafuta nafasi ya kuwa bora, kwahiyo inanilazimu kutumia ubunifu na akili nyingi ili niendelee  kuwa King of Arizona.

SWALI: Jambo gani limekufanya ujiite Mfalme wa Arizona

Emanuel Ek: Sio mimi niliamua kujiita King of Arizona ila watu walioona kazi zangu za mitindo na jinsi ninavyokubalika hapa Arizona wakaamua kunipa hilo jina na mimi nikakubali sababu nastahili hiyo heshima.

SWALI: Unatamani kufanya kazi na mastaa gani hapa Afrika Mashariki?

Emanuel Ek: Yeah hilo wazo lipo na natamani siku moja nifanye kazi na Jux na  Calisah

SWALI: Wahuni Gang ni nini?

Emanuel Ek:  ‘WAUNI Geng’ ni kitu kikubwa sana kwenye maisha yangu kwasababu ninaamini, mhuni ni mtu ambaye hakati tamaa kwenye maisha ndio maana nikaanzisha hilo ili kujipa moyo ninapopambana kwenye kazi zangu, nikiangalia nilipotoka mpaka hapa nilipo ni Mungu tu.

 SWALI: Familia yako inakupa sapoti kwenye kazi zako za fasheni?

 Emanuel Ek: Kama unavyojua familia huwa zinasapoti mtu kulingana na jambo gani anafanya, ukifanya mambo ya ovyo familia haiwezi kusapoti ujinga ila kwangu mimi nashukuru familia inanisapoti sababu nafanya kazi nzuri, napata pesa kwahiyo familia inanipa baraka zake zote. Nawaomba mashabiki wa mitindo waendelee kunisapoti na kunifuatilia mtandaoni kwa jina la Emanuel Ek, binafsi nitaendelea kuachia kazi mpya nzuri kwaajili yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles