24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mvua yaitibulia Simba Zanzibar

kikosi-cha-simbaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MVUA zinazoendelea kunyesha visiwani Zanzibar, zimetibua mipango ya kikosi cha Simba baada ya kushindwa kucheza mechi yao ya kirafiki dhidi ya Mafunzo juzi katika Uwanja wa Amaan.

Simba imeweka kambi Unguja tangu Ijumaa iliyopita ili kujiweka fiti kabla ya kuwavaa Azam FC kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kupigwa Jumapili hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa programu ya kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Jackson Mayanja, pamoja na timu hiyo kufanya mazoezi ya kujiweka fiti, pia ilipanga kucheza michezo miwili ya kirafiki.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa timu hiyo, Abbas Ally, ambaye ameambatana na timu kambini huko, alisema mvua hizo ziliwafanya  kuahirisha mchezo huo kwa kuhofia kuwepo kwa usalama mdogo wa wachezaji endapo watalazimisha kucheza katika hali hiyo.

“Tuliamua kuahirisha mchezo huu kwa kuhofia wachezaji wasije kupata majeraha, lakini endapo hali ya hewa itabadilika leo (jana), saa moja tutacheza kama ilivyopangwa,” alisema.

Alisema licha ya mvua hizo kuzuia mchezo huo, hazijaharibu programu ya mazoezi kwani timu imeendelea kujifua kama kawaida na haitasimama hata kama mvua hizo zitaendelea.

“Mazoezi yanaendelea kama kawaida kwa muda ambao mwalimu anataka, hivyo timu itaendelea kujifua hadi kesho tutakaporudi huko kusubiri mchezo,” alisema.

Simba na Azam FC zilishindwa kutambiana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza na kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles