26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Tanzania yazinduliwa K’njaro

Miss TanzaniaNA SAFINA SARWATT, KILIMANJARO

MASHINDANO mbalimbali ya kupata warembo wa kuwakilisha mikoa katika shindano la kumsaka mrembo
atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia yameanza kwa kuzinduliwa mkoani Kilimanjaro.

Katika uzinduzi huo mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga,
alisema mashindano hayo yamezinduliwa kwa mara ya kwanza mkoani humo kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa na waandaaji wake.

Alisema historia ya mashindano hayo ilianza mwaka 1994 katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuenea mikoa yote ya
Tanzania ambapo mpaka sasa mashindano 78 yameshafanyika.

Lundenga alifafanua kwamba Mkoa wa Kilimanjaro ni muhimu kutokana na idadi kubwa ya washiriki na washindi wa miss Tanzania kuwa na asili ya kutokea huko ambapo warembo 30 wakitarajiwa kushindana kumpata Miss
Kilimanjaro 2016/2017 atakayeuwakilisha mkoa huo katika mashindano ya Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles