27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Alice Kella: Wazazi hawana msaada na muziki wangu

Alice KellaNA BEARTICE KAIZA

MKALI wa kuimba katika shoo za ‘live’, Alice Kella, ameweka wazi kwamba licha ya kipaji cha kuimba alichonacho wazazi wake hawataki afanye muziki anaofanya badala yake wanamtaka aimbe muziki wa injili bila yeye kutaka.

Kutokana na hilo, mwimbaji huyo anayetamba na wimbo wa ‘Nimekuchagua’ amewaomba wazazi wasiwalazimishe
watoto wao wanachotaka wao bali wawaongoze vyema kwa wanachotaka watoto ili wafanye kwa wema na kutunza maadili yao na ya taifa lao.

“Ndoto zangu na moyo wangu unapenda muziki huu ninaofanya, lakini wazazi wangu wanataka nikaimbe nyimbo za injili ndiyo maana wazazi wangu hawanitii moyo wala kunisaidia katika muziki nifanyao kitu ambacho kinamuumiza sana kwa kuwa muziki ninaofanya unanisaidia fedha za kujikimu kimaisha.

Msanii huyo aliongeza kwamba bila baraka za wazazi wake hatoweza kufanya vema katika kazi yake ya muziki hata kama ana kipaji kikubwa pia anawataka wazazi watambue kwamba muziki siyo tabia mbaya kama wadhaniwavyo wazazi wake.

“Wazazi wangu wangenisaidia katika muziki wangu nina ndoto za kuwa zaidi ya Vanessa Mdee kwa kuwa anajua anachofanya ambacho mashabiki wake wanataka,” alimaliza Alice.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles