MWANAMUZIKI kutoka Oakland, California nchini Marekani, Antique Davis Edutainment, anatarajia
kufanya ziara ya kimuziki Julai nchini Tanzania na Hispania ambapo atatumia wiki tatu.
Mwanamuziki huyo anayeimba muziki Afro pop, Afro Beat, Reggae na Dancehall, aliliambia MTANZANIA kwamba ziara yake itaanzia nchini Ghana ambapo atatumia wiki sita kisha Tanzania na Hispania atakapotumia wiki tatu.
Katika maandalizi ya kutangaza albamu yake mpya ya ‘Remember Vol. II’ anayotarajia kutoa Juni huku asilimia kubwa ya muziki wake ukiwa umeandaliwa nchini Ghana na nchi nyingine za Afrika Magharibi.
“Kiukweli nashukuru kwa nchi za Afrika kutokana na asilimia kubwa ya muziki wangu kuandaliwa huko na sasa nina ziara ya kimuziki kwa ajili ya kutangaza albamu yangu hiyo nimepanga kutembelea, DC&Ghana na Tanzania na kisha nitaelekea Hispania,” alisema Antique.