23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Msajili avipa vyama miezi mitatu kukamilisha hesabu

mutungiNa Elizabeth Hombo, Dodoma

MSAJILI wa Vyama Siasa, Jaji Francis Mutungi amevipa vyama vya siasa  miezi mitatu kukamilisha hesabu zao.

Akizungumza   nje ya viwanja vya Bunge jana,  Jaji Mutungi alisema ukaguzi wa fedha katika vyama ni suala la  sheria na lina mchakato.

Jaji Mutungi aliyasema hayo siku chache baada Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kutoa ripoti yake ya mwaka 2014/15.

Alisema   ofisi yake imeisoma taarifa ya CAG na   inaifanyia kazi kwa kuvipa vyama hivyo miezi mitatu kukamilisha  hesabu zao.

“Kwa mujibu wa sheria tunatakiwa kuvikumbusha vyama kufanya ukaguzi na tulifanya hivyo mwanzoni mwa mwezi huu (Aprili).

Tuliviandikia barua vyama vyote. Lakini kutokana na kuibuliwa kwa suala hili tumeviandikia barua na kuvipa miezi mitatu kukamilisha hesabu zao,”alisema.

Alisema ofisi yake haiwezi kuvilazimisha vyama kuhusu suala hilo kwa vile  jambo hilo linafanyika kwa matakwa ya  sheria.

“Baada ya CAG kukagua hatua inayofuata ni kuchukua taarifa na kuangalia hatua gani zifuatwe kwa kuzingatia maelezo yake.

Mfano, kama kuna sintofahamu kwa hesabu za vyama vinavyopata ruzuku hatua mojawapo ni kukata kile kiwango kinachodaiwa katika hesabu za CAG kutoka katika ruzuku,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles