22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Lowassa, Sumaye kutua Dodoma

SumayeNa Bakari Kimwanga, Dodoma

ALIYEKUWA mgombea urais aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) mwaka jana, Edward Lowassa, na aliyekuwa mpigadebe wake, Frederick Sumaye, wanatarajiwa kuwasilia mkoani Dodoma leo.

Viongozi hao ambao ni mawaziri wakuu wa zamani, watawasili mjini hapa na kuwa na vikao na wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wanatarajia kuwapa darasa wabunge hao namna ya kukabiliana na Serikali ndani ya Bunge.

Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA jana mjini hapa kuwa vigogo hao walianza safari ya kuingia mjini hapa jana mchana.

“Ni kweli Lowassa anakuja Dodoma leo (jana) na taarifa ambazo kwa karibu tulikuwa tunawasiliana na wasaidizi wao, zinasema walikuwa wameanza safari ya kuja, tumejiandaa kwa ajili ya mapokezi ya viongozi wetu wapendwa.

“Watakapofika watazungumza na wabunge wote wa upinzani, hasa wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuwaeleza mikakati kabambe hasa katika Bunge hili la bajeti linaloendelea.

“…baada ya hatua hiyo, watakutana na viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk.

Mshinji ambaye kwa sasa yupo Dodoma,” kilisema chanzo chetu. Kuwasili kwa viongozi hao kunaelezwa ni kama mkakati wa kujiimarisha kwa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Wabunge wa upinzani kwa sasa wamegoma kuwasilisha bajeti ya kambi yao kwa madai Serikali iliyopo haiko kwa halali kwa kutotangazwa kwenye gazeti la Serikali.

MTANZANIA ilipomtafta Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kupata ufafanuzi wa viongozi hao kuwapo Dodoma, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles