28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Muhongo asitisha mashindano ya ngoma kukamilisha madarasa

Na Shomari Binda,Musoma

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amesetisha mashindano ya ngoma za asili yanatofanyika kila mwisho wa mwaka mkoani Mara ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Jimbo la Musoma Vijijini Lina upungufu wa yumba 31vya madarasa ili kuwafanya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 kuingia madarasani.

Katibu wa Mbunge huyo, Fedson Magoma ameiambia MtanzaniaDigital kuwa, kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa lakutaka wanafunzi wote kuanza masomo Januari 11, wameamua kuchukua uamuzi huo ili kushirikiana na wazazi ili kuunganisha nguvu na kuweza kutekeleza agizo hilo.

“Tumestisha mashindano ya ngoma kwa mwaka huu ili tushirikiane na wazazi kuunganisha nguvu pamoja na wadau wengine ili kukamilisha adhma ya waziri mkuu ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaingia darasani Januari 11.

“Sote ni mashahidi kwamba, suala la elimu ni muhimu, hivyo mbunge Muhongo ameamua kujikita huko kwa kipindi hiki na baadae mashindano hayo ya kukuza utamaduni yataendelea,” amesema Magoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles