28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kanisa la KCC lampongeza Rais Mgufuli

Na Allan Vicent, Tabora

Kanisa la TAG-Kitete Christian Center lililopo Manispaa ya Tabora limempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kumtanguliza Mungu katika Uongozi wake na kuliwezesha taifa kuvuka salama katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa COVID 19.

Pongezi hizo zimetolewa juzi na Askofu Mstaafu ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Rev. Paul Meivukie katika ibada ya sikukuu ya Krismas iliyofanyika jana kanisani hapo.

Alisema katika sikukuu hii ya kuzaliwa Yesu Kristo, Jamii inapaswa kumshukuru Mungu kwa mambo makubwa aliyoyafanya katika taifa letu na kwa jinsi alivyomwongoza Rais Magufuli katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19).

Alisema mioyo ya Watanzania wote inabubujika shukurani kwa Mungu kwa jinsi Rais wetu alivyosimama katika imani na kutangaza maombi ya siku tatu ya nchi nzima kuomba dua na sala na Mungu akasikia kilio chetu na kuliponya taifa.

Kwa upande wake Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo, Rev Shadrack Herman aliwataka Watanzania kuendelea kumtumaini Yesu Kristo na kumpa nafasi katika maisha yao ili awalee na kuwapitisha katika magumu yote wasiyoyaweza.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo, Dk. Zefania Zenga na Jovent William walisema kuwa Rais Magufuli ni kiongozi na mtumishi wa Mungu, imani yake imelibeba taifa na kuokoa roho za wananchi.

Walibainisha kuwa kama sio ujasiri na imani aliyonayo kwa Mungu ugonjwa wa corona usingeisha haraka kiasi hicho na watu wengi wangepoteza maisha kama inavyotokea katika mataifa mengine.

Walibainisha kuwa Mungu ni mweza wa yote hivyo wakaitaka jamii kuendelea kumtumaini katika kila jambo ili aendelee kutenda makuu ikiwemo kudumishwa amani, upendo na mshikamano hapa nchini.

Aidha waliitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona kwa kunawa mikono mara kwa mara huku wakisisitiza kumtanguliza Mungu katika kila jambo.

Aidha waliwataka waumini wa madhehebu yote ya dini kuendelea kumwombea Rais Magufuli na wasaidizi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo na  kuharakisha maendeleo ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles