26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Maswa waanza kutekeleza agizo la Majaliwa

Na Samwel Mwanga,Maswa

Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari zenye upungufu ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  wanaanza masomo baada ya shule hizo kufunguliwa  Januari 11 mwakani.

Hayo yameelezwa juzi na Mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge mbele ya Waziri wa Mufugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki mara baada ya kutembelea ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Malampaka iliyoko wilayani humo.

Amesema kuwa ili wilaya hiyo wanafunzi wote alipochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za kutwa waweze kuingia madarasani ifikapo mwezi jamuari mwakani wanaupungufu wa vyumba 10 vya madarasa  na tayari sehemu nyingi ujenzi huo uko katika hatua za mwisho.

Amesema wamejipanga kwa kutumia watendaji wa Vijiji, Kata, Madiwani na Halmashauri ya wilaya ya Maswa  kuhakikisha maeneo yote ambayo ujenzi huo unafanyika unakamilika kwa wakati ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi ambaye  hataingia darasani mara baada ya shule kufunguliwa.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri tumejipanga kuhakikisha hivyo vyumba 10 vya madarasa ambavyo tuna upungufu navyo  wilayani kwetu vinakamilika  ili shule zinapofunguliwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaingia darasani na madarasa yetu yote yatakuwa na viti na meza kwa ajili ya wanafunzi,”amesema.

Aidha, ametumia muda huo kumshukuru Waziri Mashimba kwa kuweza kuchangia  vifaa mbalimbali vya ujenzi katika miradi mbalimbali katika jimbo la Maswa Magharibi hasa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa,Vituo vya Afya na Zahanati.

Naye, Waziri Mashimba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi amesema kuwa ameridhishwa na ujenzi huo unaoendelea katika shule ya sekondari Malampaka na kuwaomba wananchi kuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo na yeye akiwa Mbunge wa jimbo hilo ataendelea kuchangia  shughuli mbalimbali za maendeleo hasa katika miundo mbinu  katika sekta ya elimu na afya.

Katika ziara hiyo mbali na kutembelea ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, Waziri Mashimba ametembelea ujenzi wa vyoo katika kituo cha Afya Malampaka,Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Malampaka B na ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Mataba na kuwataka waongeze kasi ili zianze kutumika.

“Kwa kweli nimeridhishwa sana na ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa katika shule ya sekondari ya Malampaka hivyo ni vizuri Mkuu wa wilaya tukashirikiana sote kuhakikisha tunamaliza kwa wakati na watoto wetu wanapata mahali pa kusomea hata hii miradi mingine tuhakikishe nayo inakamilika ili iweze kutumika nami nikiwa Mbunge wa jimbo hili kila mradi tuliorembelea kuna mkono wangu,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles