KLABU ya Vitoria Guimaraes ya Ligi Kuu nchini Ureno imemsajili straika wa U-20 ya Cameroon, Etienne Eto’o, ambaye ni mtoto wa mpachikaji mabao wa zamani wa Barcelona, Samuel.
Etienne (19), ametua Ureno akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Real Oviedo ya Hispania mwishoni mwa msimu uliopita.
Hata hivyo, ‘dogo’ huyo atajiunga na U-23 ya Vitoria, ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya vijana.
“Vitoria Sport Clube – Futebol, inatangaza kumsajili Etienne Eto’o mwenye umri wa miaka 19, ambaye anajiunga na U-23 inayonolewa na kocha Luiz Felipe,” inasomeka taarifa ya klabu hiyo.