KLABU ya Chelsea imeripotiwa kuingia kwenye vita ya kuiwania saini ya beki wa kati wa Villarreal na timu ya taifa ya Hispania, Pau Torres.
Chelsea, mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanataka kuliimarisha eneo la ulinzi baada ya kumwacha Kurt Zouma aliyekwenda West Ham United.
Aidha, endapo Blues watakwaa kisiki kwa Torres, bado wanamtazama kwa jicho la tatu beki wa Sevilla raia wa Ufaransa, Jules Kounde.
Itakumbukwa namna Manchester United walivyojaribu kumsajili Torres, kabla ya kuangukia kwa mlinzi wa kati mkongwe, Raphael Varane.