24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Wananchi Buchosa walilia maji

Na Anna Ruhasha, Mwanza

Mradi wa maji uliofikia  asilimia 90  umeshindwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa  maji safi na salama katika Halmashauri ya Buchosa  wilayani Sengerema mkoani Mwanza  na kuwafanya wakazi wa eneo hilo kuendelea kutaabika.

Baadhi ya wananchi katika Kijiji Cha Kamisa  kilichopo kata ya Kasisa,   Amina Rashidi  na Joshua  Kulwa wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema kuwa licha ya kuwepo mradi huo  unaotekelezwa  na wakala wa maji na usafi  mazingira Vijiji ( Ruwasa  )wilayani Sengerema mkoani hapa  bado wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika eneo hilo.

“Tunaoimba serikali ikamilishe mradi huu kwa wakati , sisi wakazi wa Kijiji hiki hatuna maji ya bomba tunatumia  maji ya visima  ambavyo vipo mbali na makazi  yetu , tunatembea mpaka kilometa  moja hadi mbili kufuata maji , mradi huu ukikamilika utatupunguzia adha hii”wamesema wananchi

Akitoa taarifa za utekelezaji  wa mradi huo Meneja  wakala wa   Maji  na Usafi wa Mazingira   Vijijini  (Ruwasa )   wilayani Sengerema  mkoani hapa  Venslaus Mosile amesema kuwa  mradi wa maji wa Kamisa  ni mradi  mdogo  unatekelezwa kwa zaidi ya sh milion 200   ambapo ukikamilika utatoa huduma kwa  kazi 400  na unategemea  kukamilika  Oktoba mwaka huu.

” Mradi huu umefikia asilimia 90  katika utekelezaji wake , na haujaanza kutoa maji ,tukisema umefikia asilimia 90 tunamaana kazi zote  ngumu tumeisha, kama kulaza mabomba ,tumebakiza kuunganisha tu na kazi hiyo ni ya wiki moja tu na huduma ya maji itanaanza kutolewa ” amesema meneja huyo.

Aidha  baadhi wajumbe wa kamati ya siasa  Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo na Katibu  wa CCM wilaya  Barnabas  Nyerembi,  wakitoa  maoni ya utekeleza wa mradi huo  hawakulizishwa na kazi ya utekelezaji wa mradi  ambapo wamesema taarifa na muonekano wa mradi bado  hauleti matumaini wa kukamilika kwa muda uliopangwa .

Agustine Makoye  Mwenyekiti wa Kamati hiyo  kwa niaba ya  wajumbe wameikataa taarifa hiyo na kumtaka meneja wa Ruwasa kuandaa taarifa sahihi  yenye uharisia na mradi huo na  kuiwasilisha katika ukaguzi ujao.

“Meneja umesema mradi huu umefikia asilimia 90 lakini hautoi  maji,hauoni kwamba  taarifa zako si sahihi, haiwezekani wananchi wa hapa wanakosa maji serikali imeleta fedha unaiambia kamati kwamba  mradi haujaanza kutoa maji , kwanini ulituleta hapa ? Sisi tunachokitaka  ni maji yatoke na sisi kama kamati tunaikataa taarifa yako,”amesema  Makoye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles