32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaalamu: Msongo wa mawazo husababisha kitambi

AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

MTAALAMU wa lishe kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Brenda Maro, amesema kuwa msongo wa mawazo kupitiliza unaweza kusababisha mtu kuwa na kitambi.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, alisema hali hiyo inatokana na homoni aina ya Cortisol zijulikanazo kama hormonal stress ambazo zinazalishwa mara baada ya mtu kupata msongo wa mawazo kupitiliza.

“Stress Hormone (Cortisol) ikitolewa kwa wingi inachangia au inachochea uhifadhi wa mafuta mwilini, hasa kwa wale wanawake ambao tayari wana maumbo makubwa ya tumboni,” alisema.

 Maro alieleza kuwa homoni hizo za Cortisol zinapozalishwa huwa zina kawaida ya kujikusanya sehemu za tumbo na kusababisha uhifadhi wa mafuta eneo hilo.

“Aina hiyo ya homoni zina tabia ya ‘ku-realocate’ sehemu za tumbo, inategemea lakini sio kila mwanamke au mwanaume anapata. Lakini kulingana na utafiti, aina hiyo ya homoni inachochea uhifadhi wa mafuta.

 “Inategemea mtu ana kiwango gani cha stress, lakini kadiri inavyozidi ndivyo uzalishaji wa homoni hizo unavyozidi pia,’ alisema.

Hata hivyo, Maro alibainisha kuwa hali hii ya vitambi vya stress inawakumba zaidi wanawake kuliko wanaume.

Maro alisema kuwa sababu nyingine za kitambi kwa wanawake hutokea baada ya kufikia kikomo cha uzazi.

“Tafiti duniani zinaonyesha wanawake wengi waliofikia kikomo cha uzazi wana ‘location’ kubwa ya mafuta tumboni.

“Kuna homoni inaitwa oestrogen, hizi huwa zinachochea mafuta sehemu za hips, lakini mwanamke anapofikia kikomo cha uzazi homoni hizo zinazalishwa kwa kiasi kidogo, hivyo kwa wanawake wengi inasababisha mafuta kuhifadhiwa tumboni ,” alifafanua Maro.

Aliwashauri watu kujiweka katika hali au mazingira ambayo yanaweza kupunguza msongo wa mawazo na pia kuzingatia aina ya vyakula ambavyo haviongezi mafuta mwilini hali ambayo itasaidia kuondokana na kitambi.

“Kuna vitu ambavyo vipo nje ya uwezo, mfano genes na hormone changes wakati wa ukomo wa uzazi, ila mengine unaweza kurekebisha kwa aina ya chakula, mazoezi na jinsi ya kudhibiti/kupunguza stress,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles