NMB kutoa mikopo ya huduma za afya

0
918

Tunu Nassor-Dar es Salaam

Benki ya NMB imezindua huduma mpya kwa lengo la kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati iliopewa jina la ‘NMB Afya loan’.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo leo Septemba 17, Kaimu Mkurugenzi wa benki hiyo, Filbert Mponzi amesema huduma hiyo mpya ni matokeo ya ushirikiano kati ya benki ya NMB na shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF).

Amesema NMB itatoa mikopo kuanzia Sh milioni mbili hadi bililioni tano wakati MCF inatoa dhamana ya asilimia 50 katika mikopo yote.

“Wanufaika wa Mkopo wa Afya ni hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati, maduka ya dawa na wasambazaji dawa ili kuwezesha kuiinua na kuboresha biashara za huduma za afya nchini,” amesema Mponzi.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa MCF Tanzania, Dk. Heri Marwa amesema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha watanzania wengi wapata huduma nafuu za afya na tiba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here