28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaa kupewa jina la changudoa aliyeuawa Ubelgiji

MAMLAKA za Jiji la Brussels, Ubelgiji, zimepanga moja ya mitaa yake ipewe jina la changudoa wa kigeni aliyeuawa nchini humo, ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi wanawake.

Taarifa zimedai mmoja ya mitaa ya Jiji hilo utaitwa Eunice Osayande, kahaba raia wa Nigeria aliyeuawa Juni, 2018, kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mteja wake.

Osayande aliondoka kwao, Nigeria, na kutua Ubelgiji mwaka 2016 baada ya kuahidiwa kuwa angekwenda kupewa nafasi ya kuigiza filamu barani Ulaya.

Kinyume cha matarajio yake, alifika Brussels na kulazimishwa kuingia kwenye biashara ya ngono akiahidiwa Pauni 38,000 za kuendesha maisha, ikiwamo kulipa kodi ya nyumba atakayokaa.

Wiki chache kabla ya kuuawa, Osayande aliyekuwa na umri wa miaka 23 wakati huo, alishawasilisha malalamiko kwa taasisi zinazopambania haki za machangudoa nchini Ubelgiji, akieleza anavyonyanyasika katika biashara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, alifikwa na umauti baada ya kuchomwa mara 17 na kitu chenye ncha kali. Kifo chake kiliibua maandamano makubwa ya machangudoa walioitaka Serikali ya Ubelgiji kuweka mazingira rafiki kwa biashara yao.

Inafahamika kuwa biashara ya ngono imehalalishwa nchini Ubelgiji lakini hakuna sheria inayolinda wahusika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles