24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Morogoro yanasa watuhumiwa 56 wa uhalifu

Na Ashura Kazinja, Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limewakamata jumla ya watuhumiwa 56 kwa kujihusisha na makosa mbalimbali ya uhalifu, ikiwemo kukutwa na silaha, nyara za Serikali pamoja na kuvujisha mtihani wa darasa la saba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani hapa, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro,Fortunatus Musilim-SACP, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni ya kupambana na uhalifu, wahalifu na wahalifu wenza na kwamba inafanyika katika wilaya zote za mkoa  huo.

Kamanda Musilim amesema Septemba 2, mwaka huu saa 4 asubuhi katika maeneo ya mtaa wa Reli Manispaa ya Morogoro, alikamatwa mtu mmoja mwanamke raia wa Canada, Michell Raggy(60), Mfanyabiashara na mmiliki wa hotel ya ACROPOL, akiwa na silaha 3 aina ya gobole zenye namba 6073A, 5048A na 5649A bila kibali.

Amesema mbali na mfanyabiashara huyo kumiliki silaha hizo bila kibali, lakini pia alikuwa akiziuza kwa jumla ya Sh 400,000 na reja reja kwa Sh 50,000 kila moja, na kwamba mtuhumiwa huyo anahojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Aidha, amesema Septemba 8, mwaka huu majira ya saa 4 usiku katika maeneo ya Nyamvisi Farm Block namba 209 kata ya Ruaha wilayani kilosa, walikamatwa watuhumiwa 5 wakiwa na nyara za serikali 3 (meno ya tembo) yenye uzito wa kilogramu 23.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Emmanuel Lameck(42) mkulima na mkazi wa Mikumi, Ally Likumbage(37) mkazi wa Mkamba, Jamal Said(36) mkazi wa kitete, Alon Posta (35) mkazi wa Simbalambede na Frank Andrea(40) mkazi wa Singalambede.

Vilevile amesema watuhumiwa wengine walikutwa na makossa ya kupatikana na pombe haramu ya moshi (gongo), mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi, kusalimisha silaha aina ya gobole, kupatikana na bhangi, pamoja na watuhumiwa 6 kuwa chini ya upelelezi kwa kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa darasa la saba uliofanyika kuanzia Septemba 8 hadi 9 mwaka huu.

Hata hivyo kamanda Musilim amesema operesheni hiyo ni endelevu, na kuwataka wote wanaojihusisha na uhalifu kuacha mara moja kwani oparesheni hiyo ya ‘Safisha Safisha Uhalifu Morogoro Washa moto haitawaacha salama’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles