MAREKANI
Mwanasiasa mwenye asili ya Somalia Ilham Omar, amevunja rekodi yakuwa mkimbizi wa kwanza katika historia kuchaguliwa kuingia Bunge la Marekani.
Ilham Omar (36) ameweka rekodi hiyo baada ya kushinda uchaguzi wa awali katika wilaya moja huko Minneapolis, Minnesota nchini Marekani.
Hata hivyo, Omar alishaweka historia ya kuwa msomali mmarekani wa kwanza kuchaguliwa katika baraza la wawakilishi wa jimbo la Minnesota, katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi.
Kwa kushinda uchaguzi wa awali jumatatu, mwanadada Ilham hatakuwa na upinzani wowote katika uchaguzi wa katikati ya mwezi November wa kuwania nafasi iliyoachwa wazi na mbunge Keith Ellison.
Pia atakuwa mkimbizi wa kwanza kuchaguliwa kuingia katika Bunge la Marekani na mwanamke wa pili muisilamu kuingia katika Bunge hilo.
Katika historia ya Marekani, mwanamke wa kwanza muisilamu alikuwa Rashida Tlaib wa jimbo la Michigan aliyechaguliwa wiki iliyopita.