23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘WANAWAKE WENGI WANATUMIA NJIA SALAMA YA UZAZI WA MPANGO’

|Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam



Imeelezwa kuwa asilimia 32 ya wanawake wanatumia njia ya kisasa ya uzazi wa mpango wakati asilimia sita wanatumia njia ya asili kupanga uzazi.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mashirika mbalimbali ya afya ya uzazi kuanzia mwaka 2015/16, umebaini kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanatumia njia salama ambayo inawawezesha kupanga mipango waliyokusudia iwe ya kielimu, kiuchumi na kijamii.

Meneja wa Utekelezaji wa Miradi wa Asasi ya Tanzania Communication and Development Centre (TCDC) James Mlali, amesema katika tafiti hizo, imeonyesha kuwa njia ya kisasa ya uzazi wa mpango ni salama kwa sababu imefanyiwa utafiti wa kitaalamu ambayo humuwezesha mama kupanga ratiba ya uzazi ili aweze kufikia malengo aliyokusudia ya kielimu na kimaendeleo.

“Tunawashauri wanawake kutumia njia ya kisasa ya uzazi wa mpango ili aweze kufikia malengo aliyokusudia yakiwamo ya kuleta maendeleo au elimu, kwa sababu tunaamini njia hii ni sslama na imefanyiwa utafiti na watalaam wabobezi,” amesema Mlali.

Aliongeza kuwa njia hiyo humsaidia mama pia kupanga uzazi kwa kutumia vidonge, sindano na kitanzi ambayo humpa mama nafasi ya kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake, Ofisa Ufuatiliaji wa Takwimu wa Shirika hilo, Nazir Yusuph amesema idadi kubwa ya wanawake wako kwenye ajira zisizo rasmi jambo ambalo linahitaji kuwapa elimu kuhusiana na suala la uzazi wa mpango.

“Wanawake wengi wanategemewa kwenye familia zao, hivyo basi wanahitaji kujiunga na uzazi wa mpango ili waweze kupata muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo,” amesema Yusuph.

Aliongeza kuwa mkakati uliopo ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua umuhimu wa kupanga uzazi hali ambayo inaweza kuwasaidia kuzaa watoto waliokusudia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles