25 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mshindi Twen’zetu Brazil kukwea pipa

Mtanzania Julai 8, 2014
Mkuu wa Idara ya Matangazo wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Kamugisha Kaihula (kushoto), akimkabidhi mshindi wa Promosheni ya Twenzetu Brazil, Wilbert Jacob, hati ya kusafiria, viza na tiketi ya kwenda Brazil kushuhudia moja ya mechi za Kombe la Dunia baada ya kuibuka mshindi. Katikati ni Meneja Masoko na Mratibu wa Promosheni hiyo, Michael Budigila. Picha na Humphrey Shao

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam

KAMPUNI ya New Habari (2006) Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, The African, Rai, Bingwa na Dimba jana imemkabidhi mshindi wa promosheni ya Twen’zetu Brazil, Wilbert Jacob mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Hati ya kusafiria, Visa, tiketi ya safari na tiketi ya kuangalia mchezo wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Brazil.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika banda la maonyesho la Sabasaba la New Habari, ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Matangazo wa New Habari, Kamugisha Kaihula.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaihula alisema Kampuni ya New Habari kupitia promosheni ya Twen’zetu Brazil iliyoendeshwa kupitia magazeti bora ya michezo nchini ya Bingwa na Dimba, ilikuwa na lengo la kuwapa fursa Watanzania hasa vijana kuweza kushiriki na watu wengine duniani furaha ya mchezo wa soka, unaochezwa na kupendwa na watu wengi duniani kwa kumpa mshindi fursa ya kwenda Brazil kushuhudia michuano hiyo.

Kaihula alibainisha kuwa, Wilbert ataondoka na ndege ya shirika la Afrika Kusini kuelekea Rio de Janeiro, ambako fainali za Kombe la Dunia zitachezwa Jumapili ijayo katika uwanja wa Maracana.

Kampuni ya New Habari inakuwa kampuni pekee kati ya kampuni za magazeti nchini, kuweza kumpeleka msomaji kuangalia tukio kubwa la kimichezo ambalo hutokea kila baada ya miaka minne na kufuatiliwa na mamilioni ya watu kote duniani.

Kwa upande wa Wilbert, ambaye ni mshindi aliishukuru Kampuni ya New Habari kwa kumwezesha kupata fursa hiyo adimu, ambayo hakuitarajia maishani na kuwataka Watanzania kushiriki katika promosheni zitakazoendeshwa na New Habari siku zijazo, kwani zinafanywa bila upendeleo na zina manufaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles