24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Vurugu zashusha demokrasia nchini

NA MWANDISHI WETU

MASHAMBULIZI ya mabomu yaliyotokea Zanzibar na jijin

Arusha Town
Arusha Town

i Arusha kwa nyakati tofauti yameshusha demokrasia ya Tanzania mbele ya uso wa dunia.

Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya mwezi Mei mwaka huu iliyotolewa wiki iliyopita na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na utafiti wa misingi ya utawala bora, uchumi na siasa ijulikanayo kama Economist Intelligence Unit (EIU).

Katika ripoti hiyo, EIU imeiorodhesha Tanzania kwenye nafasi ya 89 kati ya nchi 167 zilizofanyiwa utafiti kwenye eneo la demokrasia, ambapo imeonekana wazi nchi hii yenye sifa ya amani na utulivu duniani kuporomoka kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imejikuta ikiporomoka kwa nafasi nane kutoka nafasi ya 81 iliyokuwapo tangu mwaka 2012.

Alama za Tanzania kwenye vipimo vya awali vya demokrasia kimataifa zilikuwa ni 5.88 mwaka 2012, lakini kutokana na vurugu zilizojitokeza kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hali imekuwa tofauti, ambapo mwaka 2013 imejikusanyia alama 5.77.

Ripoti hiyo imeitaja hatua hiyo kuwa ni anguko la kwanza kwa Tanzania kwenye upande wa demokrasia tangu kuanzishwa kwa utafiti wa eneo hilo mwaka 2006.

Aidha, imezitaja sababu kubwa zilizosababisha anguko hilo kuwa ni ongezeko la hali ya kukosekana kwa utulivu kufuatia mashambulizi ya mabomu katika Jiji la Arusha ambalo limekuwa kitovu cha utalii nchini.

Mwaka jana jiji hilo lilikumbwa na mashambulizi yaliyolenga mkutano wa kampeni uliokuwa ukiendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mbali na walipuaji kulenga mkutano huo wa Chadema, pia walifanikiwa kulipua bomu kwenye sherehe za kidini zilizokuwa zikifanyika kwenye Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa uimara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar nao umeanza kuyumba kufuatia mvutano kuhusu kiwango cha mamlaka ilichonacho Zanzibar katika Muungano wa Tanzania.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa tangu mwezi Mei mwaka 2012, mapigano kadhaa yametokea kati ya polisi wa Zanzibari na wafuasi wa kundi la Uamsho.

Hali hiyo imetajwa kuongeza ugumu wa kuboresha demokrasia nchini kutokana na Serikali ya Muungano kuonekana kutotoa kipaumbele cha kufanya maridhiano na kundi hilo.

Kutokana na hali hiyo, ripoti imebainisha kuwa Tanzania inabakia kuwa miongoni mwa nchi zinazohesabika kama ‘hybrid regimes’ ikiwa na maana ya tawala dhaifu kidemokrasia.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa pamoja na kufanyika kwa chaguzi mbalimbali za kisiasa, bado hakuna uwazi katika baadhi ya mambo kama vile uwanja wa kisiasa wenye usawa kwa vyama vyote pamoja na raia hufichwa mambo yanayoendelea.

Udhaifu huo umeifanya Tanzania kuwa nyuma ya nchi za Mauritius inayoshika nafasi ya 17, Botswana inayoshikilia nafasi ya 26 na Afrika Kusini inayokamata nafasi ya 29 ambazo zote zimetajwa kufanya vizuri kwenye eneo la demokrasia.

UHUSIANO WA KIMATAIFA

Kwa upande wa uhusiano wa kimataifa, Tanzania inaelezwa kuwa inaweza kusalia katika hali ya wasiwasi kutokana na kutofurahishwa kwao kutokana na kukosekana kwa mafanikio katika vita dhidi ya rushwa.

Ripoti hiyo inafafanua kuwa hali ya Tanzania kuwa kwenye wasiwasi na wahisani wake inatokana na chama tawala CCM kutokuwa na mpango wa kushughulikia ipasavyo tatizo la ufisadi, hali inayotajwa huenda ikaibua mivutano ya mara kwa mara na wahisani.

Hata hivyo, uhusiano wa Tanzania na China, ambaye anatajwa kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara unatarajia kuendelea kuimarika.

Ziara za mwaka 2013 za Rais wa China, Xi Jinping na Rais wa Marekani, Barack Obama, zinaakisi ongezeko la mataifa ya nje yanayovutiwa na Tanzania tangu kugundulika kwa kiwango kikubwa cha gesi asili.

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Kwenye eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania imetajwa kuendelea kutangaza hadharani uungaji mkono maendeleo ya Jumuiya hiyo ingawa zipo dalili za utengamano.

Aidha, misimamo ya kizalendo inayooneshwa kwenye masuala ya ardhi na uhamiaji, yanatajwa kuwa chagizo kubwa la wasiwasi na kwamba Tanzania italazimika kuondoa wasiwasi kwenye maeneo hayo.

Hata hivyo, ripoti hiyo imejenga hofu kuwa huenda kukaibuka uwezekano wa tofauti za kimasilahi kati ya mataifa hayo matano, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuendesha harakati zao za maendeleo.

Katika miezi ya hivi karibuni Kenya, Rwanda na Uganda zimekuwa zikiendesha harakati zake za kukuza uchumi bila kuzishirikisha Tanzania na Burundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles