Nairobi Kenya
KOMANDO wa zamani wa kikosi maalumu cha SAS cha Uingereza, Meja Dominic Troulan, kwa mara nyingine amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kukabiliana kwa ushupavu na washambuliaji waliovamia hoteli ya Dusit mjini Nairobi na kuua watu 21.
Askari huyo Mwingereza, inaripotiwa kwa sasa yupo Kenya kuendesha mafunzo kwa vikosi maalumu vya nchi hiyo.
Troulan ambaye hakuwa zamu wakati wa shambulio hilo la ugaidi, akiwa amevaa gwanda kwa juu na suruali ya jinsi na shati la zambarau, alionekana katika kamera akiingia katika eneo hilo kisha kuibuka na watu aliowaokoa.
Mwaka 2013, Troulan pia aliokoa watu wengi wakati kundi hilo la Al-Shabaab liliposhambulia kituo cha biashara cha maduka ya kisasa cha Westgate mjini Nairobi.
Uso wake ukiwa umefunikwa zaidi na soksi, askari huyo alitumia bunduki iliyotengenezwa Canada na kubeba silaha nyingine aina ya Glock 9mm pamoja na kisu kwa ajili ya makabiliano ya ana kwa ana.
Anaelezwa kuwa alikuwa ametoka kwenda kununua mahitaji mjini aliposikia kuhusu shambulio hilo na kulazimika kuingia katika gari lake kuelekea eneo la tukio akiwa tayari na silaha zake.
Akifichua zaidi kuhusu ushujaa wa askari huyo, mkongwe wa SAS, Chris Ryan – ambaye alitumikia moja ya vikosi maalumu kwa miaka 10, aliliambia gazeti la Mirror kwamba askari huyo alikuwa amekwenda  kununua …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.