27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mjue komandoo aliyeongoza kuokoa mamia shambulio la Al-Shabaab Kenya

Nairobi Kenya

KOMANDO wa zamani wa kikosi maalumu cha SAS cha Uingereza, Meja Dominic Troulan, kwa mara nyingine amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kukabiliana kwa ushupavu na washambuliaji waliovamia hoteli ya Dusit mjini Nairobi na kuua watu 21.

Askari huyo Mwingereza, inaripotiwa   kwa sasa yupo  Kenya kuendesha  mafunzo kwa vikosi maalumu vya nchi hiyo.  

Troulan ambaye hakuwa zamu wakati wa shambulio hilo la ugaidi, akiwa amevaa gwanda kwa juu na suruali ya jinsi na shati la zambarau, alionekana katika kamera akiingia katika eneo hilo kisha kuibuka na watu aliowaokoa. 

Mwaka 2013,   Troulan pia  aliokoa watu wengi wakati kundi hilo la Al-Shabaab liliposhambulia kituo cha biashara cha maduka ya kisasa cha Westgate mjini Nairobi.

Uso wake ukiwa umefunikwa zaidi na soksi, askari huyo alitumia bunduki iliyotengenezwa Canada na kubeba silaha nyingine aina ya Glock 9mm pamoja na kisu kwa ajili ya makabiliano ya ana kwa ana. 

Anaelezwa kuwa alikuwa ametoka kwenda kununua mahitaji mjini aliposikia kuhusu shambulio hilo na kulazimika kuingia katika gari lake kuelekea eneo la tukio akiwa tayari na silaha zake.

Akifichua zaidi kuhusu ushujaa wa askari huyo, mkongwe wa SAS, Chris Ryan – ambaye alitumikia moja ya vikosi maalumu kwa miaka 10, aliliambia gazeti la Mirror kwamba askari huyo alikuwa amekwenda  kununua …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles