24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa usalama, DED watwangana makofi

Na Safina Sarwatt

-Mwanga

SIKU chache baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro,  Aaron Mbogho, kumsekwa ndani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Zefrin Lubuva, mkurugenzi huyo anadaiwa kuzichapa ngumi kavukavu na ofisa usalama wa wilaya ofisni kwake.

Viongozi hao wanadaiwa kupigana jana baada ya Ofisa Usalama wa Wilaya ya Mwanga, Abdi Mussa, kufika katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili masuala ya  ofisi.

Baadhi wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni watumishi wa halmashauri ambao hawakuta kutajwa majina yao gazetini, walisema   chanzo cha   mzozo huo ni kikao cha kilichokuwa kinaendelea ndani ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Inaelezwa kuwa mkurugenzi huyo alihitajika kuwapo kwenye kikao hicho lakini alimtuma mwakilishi wake.

“Mkurugenzi  hakuweza kuhudhuria kikao hicho na badala yake alimtuma mwakilishi wake.

“Lakini hilo linaonekana halikumfurahisha Ofisa Usalama wa Wilaya ambaye aliamua kumfuata ofisini kumhoji kwa nini hakuhudhuria kikao, jambo lililozua malumbano ya maneno na kusababisha kuchapana makonde,” walisema watumishi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini.

MTANZANIA ilipomtafuta kwa   simu   kupata ufafanuzi wa tukio hilo, DED Lubuva, hakukiri wala kukataa ingawa alieleza kuwapo  changamoto za uongozi wilayani humo.

“Ni kweli kwamba Wilaya ya Mwanga kuna changamoto ya  uongozi ila tuziachie mamlaka husika zifanye kazi yake,” alisema Luvuva

Alipoulizwa, Ofisa Usalama wa Wilaya ya Mwanga, Abdi Mussa kuhusiana na tukio hilo alijibu kwa kifupi na akisema, ‘si kweli’.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Aaron Mbogho alisema   hiyo taarifa alikuwa hajaipata  na kutaka atafutwe baada ya nusu saa.

Alipotafutwa baada ya muda huo hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, alisema alisema taarifa za tukio hilo zilikuwa  hazijafika ofisini kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles