27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Minaj: Hatujamwagana na Meek Mill

Minaj na MillNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop kwa wanawake nchini Marekani, Nicki Minaj, amekanusha habari zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ameachana na mchumba wake, Meek Mill.

Taarifa zilienea mara baada ya nyumba ya Meek Mill kuwa chini ya ulinzi kwa siku 90 kwa madai kwamba inatumika vibaya, hasa katika utunzaji wa silaha na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kutokana na hali hiyo, imedaiwa kwamba mrembo huyo alimwambia Mill kwamba hawezi kuishi sehemu zisizojulikana kwa siku 90 kutokana na jambo hilo, hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwa na rapa huyo.

Hata hivyo kupitia akaunti yake ya Twitter, mrembo huyo alikanusha habari hizo na kudai kwamba ni stori zisizo na uchunguzi.

“Hakuna anayejua undani wa maisha yetu, ninashangaa kuona watu wanasambaza habari zisizo na ukweli wowote, bado nitaendelea kuwa na Mill katika maisha yangu,” aliandika Nicki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles