25.5 C
Dar es Salaam
Friday, January 21, 2022

Mama Banza, mjukuu wake wazikwa makaburi ya Sinza

Banza StoneNA MWALI IBRAHIM

SAFARI ya mwisho duniani ya mama mzazi wa aliyekuwa nguli wa muziki wa dansi nchini, marehemu Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ imehitimishwa leo katika makaburi ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

Mama huyo ambaye jina lake halisi ni Khadija Jebeli, amezikwa sambamba na mjukuu wake, Sozy Jebeli, waliyepishana saa moja kuaga dunia juzi.

Mazishi hayo yaliwatia simanzi kubwa wananchi wa kada mbalimbali waliojitokeza kuwasitiri wapendwa hao katika makaburi hayo.

Mama huyo alifikwa na mauti baada ya kukamilisha mipango ya msiba wa mjukuu wake huyo wakiwa nyumbani kwake maeneo ya Sinza Vatican, ambapo baada ya kugawa majukumu kwa ndugu waliokuwa nyumbani hapo aliingia chumbani kwake na baadaye kukutwa akiwa tayari amefariki.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,789FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles