Dogo Janja: ‘My life’ utanitoa upya kimuziki

0
1201

Dogo-janja-HERIETH FAUSTINE NA RUTH MNKENI

MSANII wa miondoko ya hip hop, AbdulAzizi Abubakari ‘Dogo Janja’, amesema aina ya muziki aliofanya kwenye wimbo wake mpya wa ‘My life’ umelenga kumrudisha kwenye muziki baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

Dogo Janja alipata umaarufu kupitia wimbo wa ‘Anajua’ aliomshirikisha Madee.

“Kitu kilichonifanya nibadili uimbaji ni mtayarishaji  Cal kutoka Norway, alinitumia mdundo nilipokwenda studio nikapata melody pamoja na mistari, baada ya hapo nikaupeleka kwa uongozi ndiyo ikawa hivyo ilivyokuwa,” alisema Dogo Janja.

Wakati huo huo, Kampuni ya Lufedha Film inatarajia kutoa filamu yake mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Digital Pastor’, yenye mafundisho juu ya elimu ya dini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Salehe Hamisi ‘Lufedha’ alisema filamu hiyo ni ya 10 na itaanza kusambazwa Machi 7 mwaka huu sehemu mbalimbali za nchi.

Filamu nyingine zilizotolewa na kampuni hiyo ni ‘Sindano ya moto’, ‘Ndoa ya utata’, ‘Mafuriko’ na ‘Mume bora’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here