Mapokezi kumrudisha Ciara Afrika

0
1131

CiaraLAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris, amevutiwa na mapokezi aliyoyapata alipokuwa nchini Nigeria kwenye Uwanja wa ndege wa Lagos.

Msanii huyo alikuwa nchini humo kwa ajili ya shoo ya Musical Extravaganza inayofanyika kila mwaka jijini humo, ikiwa imeshawahi kuwashirikisha wasanii wenye majina makubwa, akiwemo Kelly Rowland na mwanamitindo Kim Kardashian.

“Nilijua shoo itakuwa ya kuvutia kutokana na mapokezi niliyoyapata tangu nikiwa kwenye uwanja wa ndege.

“Kikubwa zaidi nilifurahishwa na mashabiki  waliojitokeza kwenye shoo hiyo, walionekana kuimba baadhi ya nyimbo zangu, nimependa sana na ninaamini ipo siku nitarudi tena, naipenda Nigeria, naipenda Afrika,” aliandika Ciara kwenye akaunti yake ya Twitter.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here