33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mhasibu atupwa jela miezi sita Hai kwa ubadhirifu wa fedha

Na Upendo Mosha,Moshi

Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imemuhukumu aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo, Gerald Lyatuu kwenda jela miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa mali za umma na kughushi nyaraka.

Mhasibu huyo alitiwa hatiani kwa makosa mawili ya kughushi stakabadhi za kukusanya mapato ya Halmashauri ya Hai na kufanya ubadhirifu wa fedha za umma zaidi ya Sh milioni 10.2.

Akisoma hukumu hiyo Mei 7, mwaka huu katika Mahakama hiyo, Hakimu Hurson Kombe amesema kuwa Mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo kati ya Februari na Aprili Mwaka 2015 akiwa Mhasibu Msaidizi wa halmashauri hiyo.

“Mahakama hii imemtia hatiani Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Hai na imemhukumu kifungo cha miezi sita jela na kurejesha kiasi cha Sh milioni 10,259,000 ambapo alighushi stakabadhi za kukusanya mapato yatokanayo na ushuru wa soko kutoka kwa wazabuni,”amesema Hakimu Kombe.

Aidha, Kombe ameongeza kuwa, Mshitakiwa huyo baada ya kupatiwa fedha hizo na wazabuni hakuweza kuweka katika akaunti ya halmashauri bali alizitumia kwa manufaa yake binafsi.

“Pamoja na kumhadhibu mshitakiwa pia Mahakama inamuamuru kulipa faini ya Sh laki sita au kutumikia kifungo cha miezi nane jela kutokana na makosa mawili ya ubadhirifu,”amesema.

Hata hivyo mahtakiwa huyo aliamriwa na mahakama hiyo kulipa fedha alizo kula ndani ya miezi sita na kwamba iwe fundisho kwa watumishi wa umma kujihusisha na ubadhirifu wa mali za umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles