24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

MGODI WA MWADUI WAFUNGWA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

UONGOZI wa Kampuni  ya Williamson Diamonds Limited (WDL) umesitisha  kwa muda baadhi ya shughuli za uzalishaji  katika mgodi huo.

Taarifa ya uongozi wa mgodi huo kwa wafanyakazi jana, zilisema huduma za uzalishaji zimesimamishwa isipokuwa huduma maalumu  za ulinzi, tiba, umeme, maji, zimamoto na usafiri  unaohitajika katika huduma hizo.

Taarifa hiyo ilisema huduma za utawala  zitaendelea  kufanya kazi wakati huduma nyingine zitakazoendelea kuendeshwa na mgodi itatolewa taarifa   uzalishaji utakaporejea.

Taarifa hiyo  ilisema Kampuni ya WDL  inasubiri agizo la  kuacha kusafirisha nje almasi yake  kutoka mgodini, kifurushi namba W1-FY18.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinasema Serikali imezuia kusafirisha kifurushi hicho kwa misingi ambayo haijawasilishwa rasmi kwao licha ya kuona taarifa hizo kupitia vyombo vya habari.

“Hatuwezi kutoa maoni yoyote kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.

“Vifurushi vyote vinavyosafirishwa kwa biashara nje hukadiriwa thamani yake hapa mgodini na watumishi wa ‘TANSORT’ ambacho ni kitengo cha kukadiria thamani ya almasi na vito  wanaowawakilisha Wizara ya Nishati na Madini.

“Kifurushi kinavyosafirishwa kinapigwa mihuri miwili ya vyombo viwili vya Serikali, sisi uongozi hatuna ujuzi wanaoutumia ‘TANSORT’ wa kukadiria kwa muda malipo ya mrabaha kwa Serikali.

“Yanakamilishwa  baada ya kupatiwa matokeo halisi ya zabuni ya wazi ya almasi za WDL  na uaminifu wake unathibitishwa na TANSORT kutoka wizarani,’’ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Kamishna wa Nishati na Madini,   Benjamin Mchwampaka alisema taarifa ya mgodi huo haijafika kwake   bali ameiona kwenye mitandao ya  jamii.

Alisema mpaka sasa hawezi kujua athari za kusimamisha uzalishaji wa mgodi huo  hadi   atakapopata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi.

“Nimeziona mitandaoni, sijapata taarifa kutoka kwao wenyewe itabidi kuitafakari ikifika kesho (leo).

“Lazima niweze kujua hilo na niweze kufahamu pia athari na wamefunga  maeneo gani na athari hata kwa wafanyakazi itakuwa kwa kiasi gani ,’’alisema  Mchwampaka.

Hivi karibuni wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),   walikamata mzigo wenye madini ya almasi yenye uzito wa kilo 29, dakika tano kabla ya ndege kupaa,  huku yakiwa yameandikwa yana kilo 14.3.

Inaelezwa walioshiriki kufanya udanganyifu huo  ni watumishi wa serikali  waliopewa dhamana  ya ukaguzi na uthaminishaji katika mchakato wa kuanzia mgodini hadi kuidhinisha usafirishaji wa madini hayo nje ya nchi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango, juzi alitembelea uwanja wa JNIA kwa ajili ya kutoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP), Mganga Biswalo.

Alisema Tanzania imepigwa vya kutosha hivyo   wote waliohusika katika udanganyifu huo washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Waziri alisema wafanyakazi wote waliohusika kuanzia hatua ya uchimbaji wa madini hayo mpaka kule yanakosafirishwa, wamulikwe  na vyombo vya dola  kubaini uhalali wa mali zao wanazomiliki.

Ilielezwa kuwa  wamiliki wa mgodi wa madini hayo walisema yana thamani ya Dola za Marekani milioni 14.8, lakini baada ya uchunguzi ilibainika    thamani yake ni  Dola za Marekani milioni 29.7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles