24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mfalme Thailand amuoa mlinzi wake, amtawaza kuwa Malkia

BANGKOK, THAILAND

MFALME wa Thailand Maha Vajiralongkorn amemuoa Naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wake na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.

Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza kesho wakati atakapochukua wadhifa wake.

Mfalme Vajiralongkorn (66), alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa mno kilichotokea mwaka 2016.

Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba.

Ufalme ulisema kuwa: Mfalme Vajiralongkorn “ameamua kumpandisha cheo Jenerali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya, na atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi ya kuwa sehemu ya familia ya kifalme”.

Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kwa miaka mingi, ingawa uhusiano wao haukuwahi kukubalika rasmi.

Sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand juzi, ambapo watu wa wengine wa familia ya ufalme na washauri walihudhuria.

Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Suthida kichwani kisha baadaye wawili hao wakasaini cheti cha ndoa.

Mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Shirika la Ndege Thailand kuwa naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake kab la ya Desemba 2016 kumfanya kuwa jenerali kamili.

Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles