24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Merkel: Ulaya ipambane na ugaidi Afrika Magharibi

OUAGADOUGOU, BURKINA FASO

KANSELA wa  Ujerumani, Angela  Merkel  ameonya  kuhusu  hatari ya kuongezeka ugaidi katika  eneo  la Afrika  Magharibi na kuyataka  mataifa  ya  Ulaya  kuchukua  hatua dhidi  ya hali hiyo.

Kansela  Merkel  ameyasema  hayo  katika  siku  yake  ya  kwanza ya  ziara  ya  siku  tatu  katika  eneo hilo la Sahel, ambapo juzi aliwasili hapa akitarajia kuzitembelea Mali na Niger.

Mapambano dhidi ya ugaidi  ni suala  la  kimataifa, alisema baada ya kukutana na viongozi wa mataifa  ya Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad marufu kama G5.

Alisema tatizo lingine ni kuwa Marekani  inajaribu  kuzuia  kupatikana mamlaka ya vikosi  vya  mataifa  ya  Sahel  katika  Baraza  la Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa.

Aliahidi kuwa Ujerumani itazipatia  nchi  hizo kiasi  ya  euro  milioni  60  kwa  ajili  ya  jeshi  la pamoja kukabiliana na ugaidi

Aidha Rais  wa Burkina  Faso,  Roch Marc Kabore, ametaka  kuchukuliwe  hatua  za kutatua  suala  la  mzozo  wa  Libya.

Alisema vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  katika  nchi  hiyo  vinaathiri  eneo  lote  la Afrika  Magharibi.

Tatizo  hilo  ni  lazima  lipatiwe suluhisho, amesema  na  kuongeza  kwamba  bila  hivyo haitawezekana  kupiga hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles