31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Meya akaribisha watalii Iringa

Elizabeth Kilindi, Iringa

Kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii mkoani Iringa, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada, ametoa wito kwa watalii kujitokeza kwa wingi ili kujionea maajabu.

Ngwada ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari wanawake   kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walipomtembelea ofisini kwake ambapo amesema utalii unachangia kukuza pato la mkoa huo.

‘’Hadi  sasa tayari utalii unachangia kwa kiasi kikubwa pato la mkoa wetu kwa sababu wapo watalii wengi ambao wanakuja, wanataka kujifunza kuhusu chifu Mkwawa,kwenda Ruaha pamoja na makumbusho ambayo yanaelezea kuhusua mkoa wa Iringa’’amesema Ngwada.

Meya Ngwanda amesema mkoa wa Iringa ni mahali  pazuri kwa ajili ya kuwekeza kwa sababu ni jirani na makao makuu ya nchi.

‘’Bado tunahitaji watu wengi waje wawekeze Iringa,Halmashauri yetu ndio sehemu sahihi kwa sababu kuna maeneo ya kuwekeza hoteli,majengo makubwa kwa sababu mtu anaposhindwa kufanya jambo katika Mkoa wa Dodoma,sehemu ya  karibu ni Iringa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles