31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Makundi ya tembo yawa kivutio Ruaha

Elizabeth Kilindi, Iringa

Askari wa Hifadhi Daraja la Pili Kitengo cha Utalii, Munga Mtaiko moja ya kivutio kikubwa cha utalii  kwenye hifadhi ya Taifa Ruaha, ni tembo majike ambao ni ndugu kupenda kutembea katika makundi.

Mtaiko ameeleza hayo  wakati mbele ya  waandishi wa habari wanawake 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo  amesema tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wote wa ardhini.

‘’Tembo pia wanatabia ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta maji na malisho na kundi la tembo linaongozwa na jike ambaye ni mkubwa kuliko wote kwenye kundi husika,’’amesema Mtaiko.

Amesema tembo ukimuona ni kivutio kizuri na hata akiwa hifadhini humo huvutia.

‘’Nchi yetu umebarikiwa sana kama hapa Ruaha tembo ni wengi wakubwa na wakupendeza,niwashauri Watanzania wenzangu na wageni kutoka nje kuja Ruaha kujionea makundi makubwa ya tembo’’amesema mmoja wa waandishi waliotembelea Ruaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles