LEJENDARI wa soka la Brazil, Ronaldo Nazario, amesema PSG haitatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, licha ya kumsajili Lionel Messi.
Ronaldo, ambaye kwa sasa ni Rais wa klabu ya Real Valladolid, amesema ubora wa kikosi haupimwi kwa majina, bali kile kinachofanyika uwanjani.
“Bado ni mapema sana kutaja timu itakayochukua ubingwa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa,” amesema Ronaldo.
“Unaweza kuipata picha walau ikifika hatua ya robo fainali. PSG wana nafasi lakini kusema ni kitu kingine na kucheza ni kitu kingine.”
Aidha, alikiri kuvutiwa na staa wa PSG, Kylian Mbappe, akisema Mfaransa huyo ana sifa alizokuwa nazo enzi zake uwanjani.