24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Messi ashinda Ballon d’or 2021

Mshambuliaji wa PSG na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ameshinda tuzo ya Ballon d’or 2021 ikiwa ni mara saba kuchukua tuzo hiyo, huku Cristiano Ronaldo akichukua mara tano.

Tuzo hiyo imetolewa usiku huu jijini Paris, Ufaransa pamoja na tuzo nyingine tofauti ambapo mshambuliaji wa FC Bayern Munich, Robert Lewandowski ameshinda tuzo mpya ya mshambuliaji bora wa dunia ya Ballon d’Or.

Robert Lewandowski na mke wake

Golikipa wa PSG Gianluigi Donnarumma ameshinda tuzo ya kipa bora wa mwaka 2021 (Yachine Trophy), wakati kiungo wa Barcelona, Pedri Gonzalez amechukua tuzo ya kinda bora chini ya umri wa miaka 21 ‘Kopa Trophy’.

Alexia Putellas

Kwa upande wa wanawake ‘Women’s Ballon d’Or’ amechukua Alexia Putellas wa Barcelona, huku Chelsea ikishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles